Home Ligi Kuu KINACHOWABEBA DODOMA JIJI CHATAJWA

KINACHOWABEBA DODOMA JIJI CHATAJWA


 MBWANA Makata, Kocha Mkuu wa Dodoma Jiji amesema kuwa kinachoibeba timu hiyo kufanya vizuri ndani ya Ligi Kuu Bara ni nidhamu pamoja na wachezaji kufuata maelekezo.


Ikiwa imepanda ligi msimu huu imekuwa kwenye mwendo mzuri ndani ya uwanja kwa msimu wa 2020/21 ikiwa ipo ndani ya 10 bora.

Imecheza jumla ya mechi 21, imekusanya pointi 31 baada ya kushinda jumla ya mechi nane sawa na zile ilizopoteza na imeambulia sare tano.

Akizungumza na Saleh Jembe, Makata amesema kuwa wachezaji wake wanafuata maelekezo ndani ya uwanja jambo ambalo linawapa nguvu ya kufanya vizuri.

“Wachezaji wanapambana ndani ya uwanja kusaka matokeo hilo wanastahili pongezi pia nidhamu ni kitu cha msingi cha kufuata ndani ya uwanja kwa kuwa wanafuata maelekezo basi wanafanya vizuri.

“Ushindani ni mkubwa na kila timu ndani ya uwanja inasaka ushindi hivyo bado tuna kazi kubwa ya kufanya ili kufikia malengo ambayo tumejiwekea.

“Shukrani kwa mashabiki ambao wamekuwa wakitupa sapoti hivyo tunapenda waendelee kuwa nasi kwani mapambano bado yanaendelea,” amesema.

SOMA NA HII  NYOTA SITA WASIMAMISHWA NDANI YAPOLISI TANZANIA, RASHID JUMA WA SIMBA NDANI