Home Uncategorized BEKI TANZANIA PRISONS: TUNAKOSA UHURU KWA SASA

BEKI TANZANIA PRISONS: TUNAKOSA UHURU KWA SASA


NYOTA wa timu ya Tanzania Prisons, Salum Kimenya amesema kuwa kwa sasa wanapitia kipindi kigumu kutokana na kutopata uhuru wa kufanya mazoezi kama ilivyokuwa awali lakini wanapaswa wafanye hivyo kwa kuwa hakuna nnamna nyingine.

Kwa sasa Ligi Kuu Bara imesimama kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona ambavyo vimesababisha ligi nyingi duniani kusimama.

Akizungumza na Saleh Jembe, Kimenya amesema kuwa wanaomba hali ipite ili mambo yarudi kwenye usawa kama ilivyokuwa zamani.

“Kiukweli kwa sasa hali sio shwari ninaona kabisa kwangu mimi nakosa uhuru wa kufanya mazoezi kama zamani, ninaomba hali hii ipite ili turudi kwenye hali ambayo ilikuwa inatupa uhuru,”.

SOMA NA HII  KOCHA ALIYEPATA TABU MSIMU HUU MBELE YA YANGA LEO AMETIMIZA MIAKA KADHAA