Home Uncategorized SABABU YA MNATA KUTUA YANGA HII HAPA

SABABU YA MNATA KUTUA YANGA HII HAPA



METACHA Mnata, mlinda mlango namba mbili wa Yanga amesema kuwa sababu kubwa iliyomfanya ajiunge ndani ya Yanga ni ushindani wa namba uliokuwa ndani ya kikosi cha Azam FC.

Mnata alisajiliwa na Yanga ambapo alikuwa anakipiga Mbao FC kwa mkopo akitokea Azam FC ambao ndio walikuwa mabosi zake.


 “Nilijiunga na Yanga baada ya Azam FC kukubali kwa kuwa wao walikuwa wananimiliki na walikuwa wamenipeleka Mbao FC ili kujiweka sawa. 

“Ushindani ndani ya Azam FC ulikuwa mkubwa na haikuwa rahisi kupata nafasi ndani ya kikosi cha kwanza jambo lililosababisha pia nikaibukia Mbao FC,” amesema.

SOMA NA HII  IDD CHECHE APANIA KUREJEA NDANI YA LIGI KUU BARA