Home Uncategorized KOCHA YANGA : WACHEZAJI WALIKUWA WAMEINGIA KWENYE MFUMO

KOCHA YANGA : WACHEZAJI WALIKUWA WAMEINGIA KWENYE MFUMO

LUC Eymael, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa hesabu zake ni kuona timu yake inamaliza ikiwa nafasi ya pili jambo ambalo anaamini linaweza kufanikiwa kwa kuwa wachezaji walikuwa wameanza kuingia kwenye mfumo.

Kwa sasa Ligi Kuu Tanzania Bara imesimama kwa muda kupisha maambukizi zaidi ya Virusi vya Corona.

Eymael amekiongoza kikosi cha Yanga kwenye mechi 15 ambazo ni sawa na dakika 1,350 na kikosi chake kipo nafasi ya tatu kikiwa na pointi 51 baada ya kucheza mechi 27.

Eymael amesema:”Uzuri ni kwamba wachezaji walikuwa wameshaanza kuingia kwenye mfumo ila baada ya ligi kusimama ina maana kwamba kuna mambo pia yamesimama.

“Hesabu kubwa ni kuona namna gani inaweza kuwa hasa kwa kufikiria nafasi ya pili ambayo itawafanya wachezaji waamini kwamba wanaweza kufikia hatua ambayo itatuongeza hali ya kujiamini wakati ujao,” .

SOMA NA HII  CAVAN AKUTANA NA RUNGU LA KUFUNGIWA MECHI TATU NA FA