Home Uncategorized CAVAN AKUTANA NA RUNGU LA KUFUNGIWA MECHI TATU NA FA

CAVAN AKUTANA NA RUNGU LA KUFUNGIWA MECHI TATU NA FA


MSHAMBULIAJI Edinson Cavani anatarajiwa kukosa mechi tatu za Manchester United baada ya kukubali kosa la kutoa kauli inayoonyesha ubaguzi wa rangi.

 

Mkongwe huyo alimuita mmoja wa wafuasi wake “negrito” katika ukurasa wake wa Instagram, kauli ambayo kwa mataifa ya Ulaya inachukuliwa kama kuonyesha ubaguzi wa rangi.

 

Pamoja na adhabu hiyo, pia mshambuliaji huyo atatakiwa kulipa pauni 100,000 kwa kosa hilo mara baada ya kukiuka kanuni za Shirikisho la Soka la England (FA).


Pamoja na kupewa adhabu hiyo bado United imeitaka FA kuweka sawa kuwa Cavani siyo mbaguzi wa rangi na alitoa tamko hilo akiwa hana uelewa wa tamaduni ya sehemu husika.

 

“Edinson Cavani hakuwa na uelewa kuwa kauli yake itachukuliwa kama ubaguzi na ameshaomba radhi juu ya hilo kwa yeyote ambaye alikwazwa na kauli hilo.

 

“Alikuwa akijibu kauli ya pongezi iliyotolewa kwake baada ya kufunga bao kutoka kwa rafiki yake wa karibu, ameamua kushirikiana na FA na kutotaka kukata rufaa,” ilisema taarifa ya United.

 

Tukio hilo la Cavani lilitokea mara baada ya United kupata ushindi dhidi ya Southampton mnamo Novemba 29, 2020.

SOMA NA HII  MWADUI WABISHI KINOMAA, WAIKOMALIA GEITA