Home Simba SC SIMBA KURUDI BONGO KUWAVUTIA KASI WAARABU

SIMBA KURUDI BONGO KUWAVUTIA KASI WAARABU

 


BAADA ya kumaliza hesabu za kukusanya pointi sita mbele ya Biashara United,  leo kikosi cha Simba kinatarajiwa kurejea Bongo kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi dhidi ya Al Ahly, Waarabu wa Misri.

Simba ilianza kutwaa pointi tatu za Biashara United,  Uwanja wa Mkapa kwa ushindi wa mabao 4-0 mzunguko wa kwanza, jana Februari 18 ilikamilisha safari ya kutwaa pointi tatu, Uwanja Karume, Mara.


Ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Bernard Morrison linaifanya Simba inayonolewa na Kocha Mkuu,Didier Gomes kukamilisha hesabu ya kuchukua pointi sita mazima na kuwafunga mabao matano Biashara United.

Kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ipo nafasi ya pili na pointi 42 huku Biashara United ikiwa nafasi ya nne na pointi zake ni 32.

Inatarajiwa kukutana na Al Ahly iliyo kundi A, Februari 23, Uwanja wa Mkapa mchezo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa ndani ya dakika 90.

Gomes amesema kuwa anatambua mchezo huo utakuwa mgumu ila watapambana kupata matokeo mazuri. 

“Hautakuwa mchezo mzuri, lila timu inahitaji ushindi na malengo ni kuona tunaweza kushinda hivyo tutakamilisha kazi ndani ya uwanja,”

SOMA NA HII  BAADA YA GOLI LAKE LA TIKITAKA KUCHAGULIWA KUWA BORA CAF MSIMU HUU...PAPE SAKHO APEWA UBALOZI SENEGAL....