Home Habari za michezo BAADA YA GOLI LAKE LA TIKITAKA KUCHAGULIWA KUWA BORA CAF MSIMU HUU…PAPE...

BAADA YA GOLI LAKE LA TIKITAKA KUCHAGULIWA KUWA BORA CAF MSIMU HUU…PAPE SAKHO APEWA UBALOZI SENEGAL….


Mabao mawili aliyofunga Msenegali wa Simba, Pape Ousmane Sakho kwenye Kombe la Shirikisho Afrika msimu huu yameingia kwenye orodha ya mabao 8 bora ya msimu wa kombe hilo huku lile alilobinjuka tiktaka dhidi ya Asec likishika nafasi ya kwanza.

CAF wamechagua bao bora la kwanza la Sakho dhidi ya Asec Mimosas huku jingine ambalo limeshika nafasi ya nne ni lile alilolifunga kwa Mkapa dhidi ya RS Barkane wakati Simba iliposhinda 1-0.

Vyombo vya Habari nchini Senegal hivi karibuni, vilimtaja Sakho kuwa ni balozi wa Senegal nchini Tanzania na barani Afrika kutokana kazi aliyoifanya na Simba, akiwa mchezaji pekee kutoka nchi hiyo aliyecheza michuano ya Shirikisho msimu huu.

Sakho alijiunga na Simba Msimu huu akitokea timu iliyokuwa inacheza ligi ya kwao Senegal, ambapo toka alipojiunga na Simba amekuwa na mchango  mkubwa kwenye kikosi cha kwanza cha mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuuu Tanzania Bara.

Hata hivyo, kiwango cha mchezaji huyo kimekuwa cha kupanda na kushuka. kwani katika baadhi ya mechi Kocha Mkuu wa Simba Pablo Franco alikuwa akimtoa ‘sub’ kudhihirisha kuwa mchezaji guyo anakuwa amezidiwa na mchezo.

SOMA NA HII  KISA KUACHWA NA SIMBA ...DILUNGA AVUNJA UKIMYA...AFUNGUKA A-Z KUHUSU MKATABA WAKE...'BWALYA' ATIA NENO....