Home Habari za michezo BAADA YA KUIFANYIZIA SIMBA JANA….YANGA WATUA DAR KAMA WOTEE….MSTAA NANE WATIMKA CHAPCHAP…

BAADA YA KUIFANYIZIA SIMBA JANA….YANGA WATUA DAR KAMA WOTEE….MSTAA NANE WATIMKA CHAPCHAP…


BAADA ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba, kikosi cha Yanga kimetua jijini Dar es Salaam na kupewa ruhusa ya mapumziko ya siku nne huku wachezaji nane wa timu ya taifa ‘Taifa Stars’ wakitinga moja kwa moja kambini.

Yanga walitinga hatua ya fainali kombe la Azam Shirikisho  kwa kuwafunga watani zao Simba bao 1-0 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza likifungwa na Feisal Salum.

Timu ikiambatana na benchi la ufundi na viongozi waliwasiri uwanja wa ndege saa 3:30 asubuhi na kupokelewa na mashabiki wachache waliojitokeza huku wakitaja jina la Feisal Salim ‘Fei Toto’.

Baada ya kutua basi dogo la kijivu ikiwa na viongozi wa TFF waliwataka mastaa wote walioitwa timu ya Taifa kupanda ndani ya gari hiyo tayari kwa ajili ya kambi kujiandaa na mechi mbili za kufuzu AFCON 2023.

Wachezaji wakiongozwa na nahodha wao Bakari Mwamnyeto walijaribu kuomba ruhusa ili kuziona familia zao waligomewa na kuamuliwa wapande ndani ya gari hiyo.

Wachezaji walioitwa na kwenda kambini ni Mwamnyeto, Fei Toto, Abubakar Salum ‘Sure Boy’, Aboutwalib Mshery, Dickson Job, Kibwana Shomari, Farid Mussa na Zawadi Mauya.

SOMA NA HII  WAPINZANI WA YANGA LIGI YA MABINGWA KAZIKAZI HAINA KUPOA