Home Habari za michezo KISA MKUTANO WA DINI….MCHEZO WA SIMBA vs YANGA WAPANGIWA RATIBA MPYA…

KISA MKUTANO WA DINI….MCHEZO WA SIMBA vs YANGA WAPANGIWA RATIBA MPYA…

Simba SC vs Yanga SC

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imefanya mabadiliko ya tarehe za michezo yote ya mzunguko wa 26 wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2022/2023 pamoja na michezo mingine miwili ya mzunguko wa 22 (Geita Gold FC dhidi ya Coastal Union FC) na (Simba SC dhidi ya Young Africans SC).

Mchezo wa Simba SC dhidi ya Yanga SC uliopangwa kuchezwa Aprili 9 utapigwa Aprili 16, 2023 katika dimba la Benjamin Mkapa.

Mchezo wa Yanga SC dhidi ya Kagera Sugar uliopangwa kuchezwa Aprili 16, 2023 utachezwa Aprili 7, 2023 katika dimba la Benjamin Mkapa.

Mchezo wa Ihefu FC dhidi ya Simba SC uliokuwa uchezwe Aprili 15 sasa utachezwa Aprili 8 katika dimba la Highland Estate.

Mchezo wa Azam FC dhidi ya Mtibwa Sugar uliokuwa uchezwe Aprili 15, sasa utachezwa Aprili 8, 2023 dimbani Azam Complex.

Sababu za mabadiliko hayo ni uwepo wa tukio la mkutano wa dini Aprili 9, 2023 siku ambayo ilipangwa kwa ajili ya mchezo wa Simba SC dhidi ya Yanga SC.

Mabadiliko ya tarehe ya mchezo huo yameathiri ratiba ya michezo mingine yote ya mzunguko wa 26.

SOMA NA HII  ZRANE YUPO TAYARI KURITHI MIKOBA YA ROBERTINHO SIMBA