Mchambuzi wa Soka nchini Tanzania Edo Kumwembe, ameungana na wadau wa soka nchini waliomtupia lawama Mwamuzi Martin Saanya aliyechezesha mchezo wa Ligi Kuu kati ya Mabingwa Watetezi Simba SC dhidi ya Geita Gold FC, jana Jumatano (Desemba Mosi), Uwanja wa benjamin Mkapa.
Saanya analalamikiwa kwa maamuzi ya kukataa bao la Geita Gold FC, kwa madai mfungaji wa bao hilo alimsukuma beki wa kulia wa Simba SC Shomari Kapombe, kabla ya kuutumbukiza mpira wavuni.
Kumwembe ambaye pia ni Mwandishi wa Habari za Michezo ametoa dukuduku lake kwa Mwamuzi Saanya, akiwa kwenye kipindi cha Sports Arena kilichorushwa na Wasafi FM leo Alhamis (Desemba 02).
Kumwembe amesema: “Sanya hajadanganya ameona, ukitaka kujua ameona lile bao.. angefunga Mayele au Mugalu lingekubaliwa, sio kwamba waamuzi hawaoni lakini hizi Simba na Yanga zinalindwa sana na inaondoa ladha ya football yetu.
Pia “Namungo na Yanga, Yanga ilikuwa ni kichapo.”
Ushindi wa Mabao 2-1 umeendelea kuiweka Simba SC kwenye nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania bara ikifikisha alama 17, huku ikitanguliwa na Young Africans yenye alama 19 kileleni.