Home news NABI ANATAKA MABAO MENGI MBELE YA RIVERS UNITED

NABI ANATAKA MABAO MENGI MBELE YA RIVERS UNITED


 KOCHA Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amewaambia wachezaji wake kuwa anahitaji mabao mengi kesho mbele ya Rivers United ya Nigeria.

Yanga kwa sasa ipo kwenye maandalizi ya mwisho ya mchezo wao wa awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika ambao unatarajiwa kuchezwa kesho Uwanja wa Mkapa.

Kocha huyo ameweka wazi kwamba malengo yake ni kuona kwamba anashinda mchezo huo kwa mabao mengi licha ya kutowafahamu wapinzani wake vizuri.

“Najua tunaenda kucheza mchezo mgumu na wenye ushindani mkubwa kwa sababu ya namna wapinzani wetu ambavyo wanacheza lakini kwa kiasi fulani tunashukuru tumeweza kuwajua wapinzani wetu.

“Kikubwa ni kuona kwamba tunashinda kwa mabao mengi kwa sababu hiyo itakuwa ngao yetu hata kwenye mchezo ujao wa marudiano ingawa bado hauwezi kuwa mchezo mwepesi,” .

Kwenye mchezo wa kesho pia mashabiki wa Yanga watakuwa na fursa ya kuona namna Nabi atakavyoanzisha jeshi lake la kazi kwenye kusaka ushindi katika mchezo huo.

Ni Ditram Nchimbi na Heritier Makambo wanapewa nafasi ya kuongoza safu ya ushambuliaji katia mchezo huo huku Fiston Mayele yeye ishu ya vibali vya kazi ikiwa ni kikwazo kwake.

Wengine ni Shaban Djuma huyu ni beki pamoja na Khalid Aucho huyu ni kiungo nao pia wanatatizo la kutokuwa na ITC.

SOMA NA HII  KUHUSU MZIZA NA NAMNA ANAVYOCHEZA YANGA...NABI KATIKISA KICHWA WEE..KISHA AKASEMA HAYA...