Home Habari za michezo KUHUSU KIPOGO CHA SHABIKI WA YANGA, UONGOZI WACHUKUA MAAMUZI HAYA

KUHUSU KIPOGO CHA SHABIKI WA YANGA, UONGOZI WACHUKUA MAAMUZI HAYA

Klabu ya Yanga SC, imesema inatarajia kuandika barua rasmi ya malalamiko kwenda kwa vyombo vinavyohusika na mpira kuhusiana na tukio la shabiki wao kupigwa uwanjani na mashabiki wanaoaminika kuwa ni wa Simba.

Tukio hilo linadaiwa kutokea Jumamosi iliyopita wakati Simba akipepetana na Ihefu FC na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-1.

Afisa Habari wa Yanga SC, Ali Kamwe amesema kama klabu wameliona tukio hilo na wanatarajia kuandika barua rasmi ya malalamiko.

“Tutaandika barua rasmi na kufikisha kwenye vyombo husika. Lakini sisi pia wasemaji tunapaswa kuwa makini sana na kauli zetu, nilisikia mmoja anasema sisi tena sio watani wao, badala yake tunapaswa kuuenzi utani na si vinginevyo,” alisema Kamwe.

SOMA NA HII  KOCHA AL AHLY ALALAMIKA WAPITA NJIA KAMA ZA SIMBA