Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI IJAYO YA LIGI…AZAM FC WAKISIKIA HILI LA MAYELE…SIDHANI KAMA YANGA...

KUELEKEA MECHI IJAYO YA LIGI…AZAM FC WAKISIKIA HILI LA MAYELE…SIDHANI KAMA YANGA WATATOKA SALAMA…


Mshambuliaji wa Yanga SC, Fiston Mayele, amesema kuwa, malengo yao ni kuhakikisha wanaendelea kupata matokeo mazuri katika mchezo ujao dhidi ya Azam FC, huku yeye akisema anataka kufunga tena.

Yanga SC wanatarajiwa kuwa wenyeji wa Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuchezwa Septemba 6, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

Mayele alisema: “Mchezo ujao tunakwenda kucheza na Azam FC, ni mchezo mzuri na mgumu, malengo yetu ni kuhakikisha tunashinda kama ambavyo tumeanza ligi kwa kushinda michezo yetu miwili iliyopita.

Azam FC nakumbuka msimu uliopita niliifunga katika michezo yote, msimu huu nataka kuona naifunga tena kwa ajili ya kuisaidia timu yangu ishinde japo naamini haitakuwa rahisi.”

Msimu uliopita kwenye Ligi Kuu Bara, Mayele alipocheza dhidi ya Azam, mechi ya kwanza alifunga bao moja dakika ya 36 wakati Yanga ikishinda 2-0 Uwanja wa Mkapa, ilikuwa Oktoba 30, 2021. Lingine lilifungwa na Jesus Moloko dakika ya 74.

Katika mchezo wa mzunguko wa pili, Mayele pia alifunga bao moja dakika ya 78 likiwa la ushindi wakati Yanga ikishinda 2-1 ugenini Uwanja wa Azam Complex, Dar.

Ilikuwa Aprili 6, 2022. Azam bao lao lilifungwa na Rodgers Kola dakika ya 10, huku lile lingine la Yanga likifungwa na Djuma Shaban dakika ya 17 kwa penalti.

Sambamba na hilo Mayele ameongeza mkataba wa miaka minne wa kuendelea kuicheza Yanga na kuzima tetesi zote zilizodai huenda angeondoka kwenye klabu hiyo.

SOMA NA HII  KABLA YA KRISMASI...CHAMA KUTUA SIMBA...SAKHO, NYONI, WAWA NA ABDULSWAMAD KUTEMWA...ISHU IKO HIVI...