Home Habari za michezo BENDERA YA TANZANIA YAZIDI KUPEPEA AFRIKA…TWIGA STARS WAANZA KUGAWA DOZI MASHINDANO MAKUBWA...

BENDERA YA TANZANIA YAZIDI KUPEPEA AFRIKA…TWIGA STARS WAANZA KUGAWA DOZI MASHINDANO MAKUBWA …


Mabingwa watetezi, Tanzania wameanza vyema michuano ya COSAFA kwa wanawake baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Comoro mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Madibaz mjini Port Elizabeth, Afrika Kusini.

Mabao ya Twiga Stars yamefungwa na Donisia Minja dakika ya 13 na Enekia Kasonga ‘Lunyamila’ mawili dakika ya 41 na 52.

Baada ya mechi hiyo, nyota wa Twiga Stars Enekia Kasonga ‘Lunyamila’ alipewa Tuzo ya Mchezaji Bora kwa soka nzuri aliyoonyesha huku akitoa mchango mkubwa kwa ushindi wa timu yake kutokana na kufunga mara mbili.

SOMA NA HII  HUYU HAPA KIUNGO HATARI WA SIMBA...MFAHAMU KIUNDANI ZAIDI...ATAKAYE WAUA YANGA