Home Habari za michezo SIMBA NA TEMBO KUMALIZANA RASMI KESHO….NI ‘SHOW YA MBUGANI’ HII…

SIMBA NA TEMBO KUMALIZANA RASMI KESHO….NI ‘SHOW YA MBUGANI’ HII…

FT:Simba 1-0 Jamhuri

KIKOSI cha Simba ikishuka dimbani kesho dhidi ya Tembo FC ya Tabora katika mchezo wa hatua ya 32 bora ya Kombe la Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF), utakaopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam, saa 1:00 usiku.

Simba itashuka dimbani kwa mara ya kwanza tangu Januari 13 ilipocheza mechi ya fainali ya Kombe la Mapinduzi mjini Zanzibar na kufungwa bao 1-0 dhidi ya Mlandege, lakini pia itakuwa ni mara ya kwanza kwa mashabiki wa Dar es Salaam kuiona timu hiyo tangu ilipocheza mechi yake ya ligi, Desemba 23 mwaka jana dhidi ya KMC na kutoka sare ya mabao 2-2.

Wanachana na mashabiki wa timu hiyo wanatarajiwa kuonekana kwa mara ya kwanza wachezaji wao waliosajiliwa kwenye dirisha dogo la usajili ambao ni, Edwin Balua, Pa Omar Jobe, Fredy Michael ambao hawakucheza katika mechi za kombe la Mapinduzi na Salehe Karabaka, Babacar Sarr na Ladack Chasambi ambao wamefanikuwa kuonekana baadhi ya mechi hizo.

Simba inahitaji ushindi katika mchezo huo ambao ni wenyeji wa mchezo huo dhidi ya Tembo katika dimba la Azam Complex, uliopo Chamazi Dar-es-Salaam, saa 1:00 usiku.

Katika mchezo wa kesho kikosi cha Wekundu hao wa Msimbazi kinachonolewa na Kocha Abdelhak Benchikha anatarajia kufanya mabadiliko madogo huku nyota wapya wakitarajiwa kuonekana katika mchezo wa leo.

Benchikha amesema hautakuwa mchezo rahisi kwa sababu hawafahamu wapinzani wao na wanahitaji kupata ushindi lakini pia anatumja mchezo huo kutengeneza muunganiko wa kikosi chake kwa nyota wapya na walikuwepo awali.

Amesema wanahutaji kupambana kuhakikisha wanapata matokeo mazuri lakini kuwapa nafasi wachezaji wapya kuonyesha kile ambacho amewapa katika uwanja wa mazoezi.

“Haitakuwa mechi rahisi kwa sababu tunacheza na mpinzani hatumfahamu, tutacheza kumuheshimu Tembo FC , Simba ni timu kubwa na tunahitaji kuingia na mbinu za ushindi ili kusonga katika hatua inayofuata,” amesema Kocha huyo.

Ameongeza kuwa anaimani ni mchezo ambao utakuwa na mabadiliko madogo ya kikosi chake kulingana na wachezaji wao waliokuwa timu za Taifa wamechelewa kuungana na kikosi cha timu hiyo katika program ya mechi hiyo

Benchikha amesema pia mechi hiyo anaitumia kwa ajili ya kuandaa timu yake kuelekea mechi zinazokabili za ligi kuu Tanzania Bara ikiwemo dhidi ya Mashujaa FC na Tabora United zote wanaenda kucheza ugenini.

Naye kocha wa Tembo FC, Ramadhan Kilobi, amesema wanafahamu Simba ni timu kubwa ndani na nje ya uwanja, lakini hawataingia kinyonge badala yake watapambana kutafuta matokeo mazuri.

Amesema kwa muda mrefu wamekuwa katika maandalizi mazuri ikiwamo mechi za kirafiki dhidi ya Tabora United ambapo walifungwa mabao 3-1, lakini baada ya hapo walirejea mazoezini na kusawazisha makosa yote.

“Tulipoteza mchezo wetu wa kirafiki mbele ya Tabora United, baada ya hapo tukafanyia kazi madhaifu yote ambayo yalionekana na tupo imara kila upande kuhakikisha tunaifunga Simba,” amesema kocha huyo.

SOMA NA HII  MIQUISSONE AINGIA MISRI NA GUNDU...AL AHLY YAPOTEZA TAJI MBELE YA ZAMALEK