Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI YA KESHO…BENCHIKHA ‘KUUWA MENDE KWA NYUNDO’….

KUELEKEA MECHI YA KESHO…BENCHIKHA ‘KUUWA MENDE KWA NYUNDO’….

Habari za Simba leo

Kocha Mkuu wa Simba SC, Abdelhak Benchikha ameahidi kufanya mabadiliko ya kikosi cha timu hiyo katika mchezo wa Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ dhidi ya Tembo FC utakaochezwa keshokutwa Jumatano (Januari 31) katika Uwanja wa Azam Complex, Dar es salaam.

Mabadiliko hayo ni baada ya baadhi ya nyota wake waliokuwa kwenye majukumu ya timu zao za Taifa katika Fainali za Mataifa ya Afrika ‘AFCON 2023’ zinazoendelea nchini Iavory Coast, ambapo kwa Tanzaniani Aishi Manula, Mohammed Hussein Tshabalala’, Mzamiru Yassin na Kibu Denis, huku kwa Zambia akiwa Clatous Chama ambao wanatarajiwa kujiunga na timu yao kuanzia jana Jumatatu (Januari 29) baada ya kutolewa katika hatua ya makundi.

Hata hivyo, ataendelea kumkosa beki kisiki cha Wekundu wa Msimbazi hao, Enock Inonga Baka, ambaye timu yao ya Taifa ya DR Congo, imetinga hatua Robo Fainali ya fainali hizo zinazoendelea nchini Ivory Coast.

Akizungumza jijini Dar es salaam, Kocha huyo amesema anategemea kufanya mabadiliko ya kikosi chake kuelekea katika mchezo wao ujao wa ASFC dhidi ya Tembo ambao utamsaidla kuandaa kikosi rasmi kwa ajili ya michezo iliyopo mbele yao, Ligi Kuu Tanzania Bara na Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Amesema licha ya kutokuwapo kwa nyota muhimu ambao wako kwenye majukumu ya timu za taifa na wengine kujiunga hivi karibuni baada ya kutolewa, lakini haitaathiri mipango ya mbinu zake kuelekea mchezo huo wa ASFC.

“Kuna baadhi ya wachezaji hawakuwapo kwenye maandalizi ya mechi yetu ijayo ya Kombe la Shirikisho ‘ASFC’, tulioanza nao wanajua umuhimu wa mchezo huo, mabadiliko yatakuwapo madogo kwa sababu ya kuwapa nafasi nyota wapya, lakini tukichanganya na wale waliopo mwanzo.

“Ninapambana kwa moyo wote kwa ajili ya kushinda kila siku, Simba SC tupo kwenye michuano ya CAF ambayo nataka tufike mbali zaidi ya matarajio ya wengi, lakini ubingwa wa ligi ni muhimu lazina tufanye vizuri tushinde,” amesema kocha huyo kutoka nchini Algeria.

Ameongeza kuwa yupo Simba SC kuendelea kufanya kazi yake kwa jitihada zote kuhakikisha wanaendeleza furaha kwa mashabiki wao na kufikia kile ambacho kinatararajiwa na Wanasimba katika kila mechi iliyopo mbele yao.

Kuhusu nyota wapya, amesema anategemea kuwapa nafasi katika mechi dhidi ya Tembo akitumia mchezo huo kutafuta matokeo mazuri pamoja na kupata muunganiko wa wachezaji wapya na waliokuwapo tangu awali.

Naye Meneja ldara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally, amesema kuanzia jana Jumatatu na leo Jumanne baadhi ya wachezaji waliokuwapo kwenye timu za taifa watajiunga na wenzao kwa ajili ya kujiandaa na mechi zijazo za ligi na michuano ya kimataifa.

SOMA NA HII  MECHI HII YA YANGA YAPELEKWA MBELE...HUYO NABI SASA!!