Home Habari za michezo MECHI HII YA YANGA YAPELEKWA MBELE…HUYO NABI SASA!!

MECHI HII YA YANGA YAPELEKWA MBELE…HUYO NABI SASA!!

MECHI HII YA YANGA YAPELEKWA MBELE...HUYO NABI SASA!!

Bodi ya Ligi Kuu itaupangia tarehe nyingine mchezo wa ligi kuu kati ya Singida BS dhidi ya Yanga ambao ulipaswa kupigwa mwishoni mwa wiki
Yanga inatarajiwa kusafiri nchini Nigeria kwa ajili ya mchezo wa mkondo wa kwanza robo fainali kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Rivers United utakaopigwa Jumapili April 23

Mchezo wa marudiano utapigwa April 30 katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Baada ya Singida BS, mchezo utakaofuata ni dhidi ya Dodoma Jiji ambao utapigwa uwanja wa Azam Complex, Chamazi

Ratiba ya mchezo huo nayo huenda ikaathiriwa kutokana na ratiba ta mechi za CAF

Yanga itakwenda kuhitimisha msimu mkoani Mbeya kwa mechi mbili dhidi ya Mbeya City na Tanzania Prisons

Katika mechi nne zilizosalia, Yanga inahitaji alama nane ili kitetea ubingwa kwa msimu wa pili mfululizo

Wananchi pia wanakabiliwa na mchezo wa nusu fainali kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) dhidi ya Singida BS ambao utapigwa uwanja wa Liti, Singida

SOMA NA HII  KISA KOSA KOSA ZA KINA KAGERE,....KOCHA SIMBA KAAMUA KUWATOLEA UVIVU...AFUNGUKA WALICHOFANYIWA...