Home Habari za michezo NI SIMBA SC TENA….CAF KUTUMA WATAALAMU KUJA KUFANIKISHA JAMBO MECHI NA WYDAD…

NI SIMBA SC TENA….CAF KUTUMA WATAALAMU KUJA KUFANIKISHA JAMBO MECHI NA WYDAD…

Habari za Simba SC

Kesho kutwa Alhamisi wataalamu wa teknolojia ya Video Assistants Referee (VAR) kutoka Misri wanatinga nchini tayari kwa kufunga mitambo yao na kuijaribu kwa ajili ya mechi ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika itakayozikutanisha Simba SC na Wydad Casablanca ya Morocco, Jumamosi hii.

Hii itakuwa ni kwa mara ya pili katika Historia kwa VAR kutumika Tanzania katika Uwanja wa Benjamin Mkapa na mara zote ni Simba SC pekee wametumia VAR.

Kwa mujibu wa CAF kuanzia hatua ya Robo Fainali Teknolojia ya VAR inatumika katika michezo ya Ligi ya Mabingwa.

Simba  wanaikaribisha Wydad katika Uwanja wa Mkapa mchezo wa Mkondo wa kwanza hatua ya Robo Fainali Aprili 22.

SOMA NA HII  WAKATI USAJILI BONGO UKIZIDI KUCHANGANYA MOTO...STEPHEN SEY WA NAMUNGO AITWA TENA TZ NA WAKUBWA...