Home Simba SC HAWA HAPA NYOTA WA SIMBA MIKATABA YAO INAMEGUKA

HAWA HAPA NYOTA WA SIMBA MIKATABA YAO INAMEGUKA


WAKATI ishu ya mkataba wa beki wa kushoto, mzawa Mohamed Hussein, ‘Tshabalala’ likizidi kufukuta ndani ya Simba inaelezwa kuwa kuna nyota wengi ndani ya kikosi hicho ambao mikataba yao inatarajiwa kumeguka mwisho wa msimu huu.

Habari zinaeleza kuwa tayari mabosi wa Simba wameanza kufanya vikao ili kujua namna gani wanaweza kuwaongezea mikataba nyota hao ambao wamekuwa na mchango mkubwa ndani ya kikosi hicho.

Miongoni mwa nyota ambao mikataba yao ipo ukingoni ni pamoja na kiungo mkabaji, Jonas Mkude.

Kiungo mshambuliaji, Miraj Athuman.

Kiungo mkaabaji Mzamiru Yassin.

Beki mkongwe na kiraka ndani ya Simba, Erasto Nyoni.

Beki wa kati, Pascal Wawa.

Beki wa kushoto, Mohamed Hussein.

Kiungo mshambuliaji, Francis Kahata.

Mshambuliaji namba moja wa Simba Meddie Kagere mwenye mabao 11.

Nahodha wa Simba, mshambuliaji mzawa John Bocco mwenye mabao 10.

Beki  Shomari Kapombe

SOMA NA HII  KAPOMBE KUIKOSA DODOMA JIJI LEO JAMHURI