Home Yanga SC ISHU YA TONOMBE KUSEPA YANGA IPO NAMNA HII

ISHU YA TONOMBE KUSEPA YANGA IPO NAMNA HII


 HATIMAYE baada ya kiungo wa Yanga, Tonombe Mukoko kuhusishwa kuhitajika na miamba ya soka kutoka Afrika Kusini, Kaizer Chiefs, kiungo huyo ameweka wazi ishu hiyo huku yeye mwenyewe akisema kuwa taarifa hizo anazisikia kama tetesi.

 

Mukoko amesema kuwa yeye kama mchezaji amekuwa akisikia tetesi mbalimbali kuhusu kutakiwa na Kaizer Chiefs lakini yeye hajui lolote kwani kama ikitokea anatakiwa kuuzwa basi Yanga ndio wanahusika kwa kuwa yeye bado ana mkataba na Wanajangwani hao.

 

“Kuhusu kuhitajika na Kaizer Chiefs, nimesikia taarifa hizo, lakini kwangu sifahamu lolote kabisa kwani kila kitu kuhusu mimi kipo katika mikono ya Yanga, kwa kuwa bado nina mkataba nao.


“Hivyo ikitokea nimeuzwa basi fahamu Yanga ndio watakuwa wameniuza, bado mimi ni mchezaji wa Yanga na nitaendelea kuwa hapa, kwa sasa ninaangalia namna gani pamoja na wachezaji wenzangu tunapambana kwa ajili ya kuipatia mafanikio timu, ikiwemo kutwaa ubingwa,” amesema mchezaji huyo.

 

Kiungo huyo kwa sasa yupo ndani ya ardhi ya Bongo kwa kuwa alikuwa na timu ya Taifa ya DR Congo iliyocheza michezo miwili dhidi ya Gabon na Gambia katika kuwania tiketi ya kufuzu Afcon ila iliishia hatua ya makundi.

SOMA NA HII  BAADA YA YANGA KUBEBA UBINGWA....MANARA AIBUKA NA HILI KUHUSU INJINIA HERSI...ADAI BILA YEYE HAKUNA KITU..