Home news EMMANUEL OKWI ATOROKA KAMBINI MISRI

EMMANUEL OKWI ATOROKA KAMBINI MISRI


 NYOTA wa timu ya Al Itihad FC ya Misri na staa wa zamani wa Klabu ya Simba, Emmanuel Okwi inaelezwa kuwa hayupo kwenye kambi hiyo kwa muda wa mwezi sasa. 

Raia huyo wa Uganda ambaye ni nahodha pia wa timu ya Uganda, Okwi inaelezwa kuwa yupo kimya mpaka sasa kuhusu kurejea kambini.

Kwa mujibu wa tovuti ya Korabia.Com ya nchini Misri ilimnukuu Rais wa Klabu ya Al Ittihad, Mohamed Mousely baada ya mchezo wa timu hiyo dhidi ya Ismaily wakishinda 2-1.

Mohamed alisema:”Kuna wachezaji akiwemo Okwi hawapo kambini, wametoroka kwani tumewatumia barua lakini bado kimya, walikwenda kwenye timu zao za taifa lakini hawajarudi hadi sasa,”.

Ripoti nyingine zilidai kuwa Okwi ameamua kutorejea kwenye klabu yake hiyo kwa kuwa mkataba wake ulimalizika Juni 31 mwaka huu na hakukuwa na mazungumzo ya kumuongezea dili jipya.

Okwi amefanikiwa kufunga mabao matatu katika mechi 17 alizocheza ndani ya msimu huu.

SOMA NA HII  PAMOJA NA KUONGOZA WENYE MAGOLI MENGI BONGO...MPOLE KAMA KAWAIDA YAKE...KAJA NA HILI JIPYA....AMKANA MAYELE...