Home Yanga SC ISHU YA NIYONZIMA KUIPIGA CHINI RWANDA IKO HIVI

ISHU YA NIYONZIMA KUIPIGA CHINI RWANDA IKO HIVI


KIUNGO wa klabu ya soka ya Yanga na timu ya Taifa ya Rwanda, Haruna Niyonzima amesema kuwa hajafikia uamuzi wa kustaafu kuichezea timu ya taifa ya Rwanda kama ambavyo vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti.

Niyonzima hivi karibuni akiwa kwenye mahojiano na wanahabari nchini Rwanda alinukuliwa akisema anatarajia kuachana na kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo.

Niyonzima amekuwa ndani ya kikosi cha timu ya Taifa ya Rwanda kwa muda wa miaka kumi mpaka sasa huku akiwa tayari ameichezea timu hiyo zaidi ya michezo 100.

AkizungumzIA msimamo wake katika hilo, Niyonzima amesema: “Watu wengi hawakunielewa vizuri nini nilitaka kuwasilisha katika maelezo yangu kuhusu kuichezea timu ya Taifa niliyoyatoa hivi karibuni.

“Nilichotaka kumaanisha ni kwamba, iwapo Rwanda ingefanikiwa kufuzu kucheza michuano ya AFCON ya mwakani basi baada ya michuano hiyo ningestaafu.

“Lakini kwa kuwa kwa bahati mbaya hatujafanikiwa kufuzu, basi siwezi kufanya hivyo kwani bado kuna malengo yangu binafsi ambayo nataka niyatimize nikiwa na kikosi cha timu yetu ya Taifa.

SOMA NA HII  ENG HERSI USO KWA USO NA BOSI WA MBAPPE UFARANSA....WALICHOTETA HIKI HAPA...