Home news AMBOKILE: NITAUWASHA MOTO ZAMBIA

AMBOKILE: NITAUWASHA MOTO ZAMBIA


BAADA ya kukamilisha usajili wa kujiunga na kikosi cha Nkana kwa mkataba wa mwaka mmoja, mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Eliud Ambokile amesema kuwa ana mategemeo makubwa ya kufanya vizuri akiwa nchini Zambia.

Tangu ajiunge na TP Mazembe mwezi Juni, 2019 Ambokile amekuwa na wakati mgumu kupata nafasi ndani ya kikosi cha kwanza ambapo kwa msimu huu pekee hajacheza mchezo wowote kwenye Ligi Kuu ya DR Congo.

Akizungumzia mipango yake baada ya kukamilisha usajili huo, Ambokile amesema: β€œNi kweli nashukuru Mungu kwa kukamilisha usajili wangu wa kujiunga na klabu ya Nkana ya Zambia kutokea Mazembe.

β€œNkana wamenisajili kama mchezaji huru na tayari nimesaini mkataba wa mwaka mmoja, ni matumani yangu baada ya kukosa nafasi ya kucheza nikiwa na Mazembe, nitapata nafasi ya kuonyesha uwezo wangu ndani ya kikosi cha Nkana,”

SOMA NA HII  TFF NA TBC YAINGIA MKATABA WA MIAKA 10 KWA MATANGAZO