Home news HII HAPA TIMU MPYA MATAJIRI WA LIGI DARAJA LA KWANZA INAYOTAKA ...

HII HAPA TIMU MPYA MATAJIRI WA LIGI DARAJA LA KWANZA INAYOTAKA KUMSAJILI HAMIS TAMBWE


DTB FC inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza, imethibitisha nia yao ya kumrudisha nchini straika maarufu Mrundi, Amissi Tambwe.

Tambwe aliyewahi kucheza katika klabu za Simba na Yanga anasifika kwa utupiaji nyavuni na Katibu Mkuu wa DTB, Muhibu Kanu amesema; “Ni kweli tuko kwenye mazungumzo, tukikubaliana atakuja.”

Habari za uhakika kutoka kwa mtu wa karibu na mchezaji huyo alilidokeza  kwamba Tambwe anarejea nchini wakati wowote kuanzia jana baada ya kumalizana kila kitu na mmoja wa vigogo wa timu hiyo.

“Tambwe anarejea nchini kuanzia wiki hii, ameshaelewana kila kitu na bosi wa timu hiyo na anakuja kusaini mkataba, ameamua kuja huku kwa sababu ameona timu hiyo inajipanga kupanda Ligi Kuu,” kilisema chanzo hicho.

Wakati huo huo, inaelezwa vigogo wa klabu hiyo wapo kwenye mipango ya kumrejesha nchini Tafadzwa Kutinyu, raia wa Zimbabwe aliyewahi kucheza Singida United na Azam FC.

SOMA NA HII  SIMBA KWA MISIMU MIWILI SASA WAMESHINDWA NA WATANI ZAO