Home Habari za Yanga Leo AZIZ KI AIPA THANK YOU YANGA…AWATAJA WACHEZAJI WENZAKE

AZIZ KI AIPA THANK YOU YANGA…AWATAJA WACHEZAJI WENZAKE

Habari za Yanga leo

KIUNGO MSHAMBULIAJI wa Yanga SC Stephen Aziz Ki ametoa shukrani zake za dhati, kwa Uongozi wa klabu hiyo pamoja na wachezaji wenzake kwa kukamilisha mafanikio na malengo ya msimu uliomalizika.

Azizi Ki ambaye ni mfungaji bora wa Ligi Kuu ya NBC, akiwa amefunga mabao 21 na kutoa pasi za magoli 8, amehusika kwenye magoli 29 ya Yanga kwa msimu wa 2023/24 kwa upande wa Ligi Kuu pekee.

Kupitia ukurasa wake wa wa Instagram Master Ki kama wenyewe wanavyopenda kumuita, ameandika ujumbe huu kwenda kwa Viongozi, Wachezaji na Mashabiki wa Yanga.

“Kila kitu kiliwezekana, Asante kwa wachezaji wenzangu, wafanyakazi, benchi na ufundi na Rais hasa wewe (Eng Hersi), mashabiki, wapendwa wangu na pia familia kwa baraka za MUNGU mwema”

“Kwa mara nyingine tena Asante kwa uaminifu wako, msaada wako, imani yako, umenipa mengi katika msimu mzima” Ameandika Stephen Aziz Ki.

Kiungo huyo Raia wa Bukinabe (Burkina Faso) amekuwa na kiwango bora sana tangu atue mitaa ya Jangwani kwa wananchi, na hii imepelekea kuwa ni miongoni mwa mastaa wanaolipwa pesa ndefu zaidi hapa Bongo.

Mshahara wa Azizi Ki unakadiriwa kuwa ni Tsh Milion 27 kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali.

Mchezaji huyo pia anapewa nafasi kubwa zaidi ya kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Ligi Kuu ya NBC, kinachosubiriwa tu ni siku ya ugawaji wa hizo tuzo.

SOMA NA HII  GAMONDI AFUNGUKA HAYA MALIPO UBINGWA PAWEKWA WAZI