Home Habari za Yanga Leo BAADA YA AZIZ KI KUAGA…AFUATA GAMONDI…INSHU YAKE IKO HIVI

BAADA YA AZIZ KI KUAGA…AFUATA GAMONDI…INSHU YAKE IKO HIVI

Habari za Yanga- Miguel Gamondi Yanga

UONGOZI wa Yanga Chini ya Eng Hersi Said umeendelea kufanya vikao na Kocha Mkuu wa timu hiyo, Miguel Gamondi aliyemaliza mkataba ili asalie kikosini, wakati huo Gamondi akipiga hesabu za kuondoka kwenda kutafuta changamoto nje ya klabu hiyo.

Yangailimpa Gamondi mkataba wa mwaka mmoja, akichukua nafasi ya Nasredine Nabi na sasa wanapambana kuhakikisha inamuongezea mkataba kutokana na mafanikio aliyoipa timu hiyo, lakini mambo bado ni magumu huku akihusishwa zaidi na klabu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.

Vileville tunatambua kwamba Muargentina huyo ana ofa nyingine kutoka hapa Tanzania, moja ya timu kubwa tu imempa nafasi ya kuwa kocha mkuu.

Miguele Gamondi hivi karibuni wiki iliyopita, alinukuliwa akisema kwamba;

“Makocha tunapita. tunachotaka kufanya ni kuacha alama muhimu kwa klabu na kufikia mafanikio,” alisema Gamondi katika mahojiano ya wazi na wanahabari na kungeza;

“Nataka kufikiri na kujadili kwani mkataba wangu unamalizika leo (juzi).” Hata hivyo, Mwanaspoti lilienda mbali na kumtafuta kocha huyo kumuuliza kuhusu ofa aliyonayo kutoka kwa Kaizer Chiefs na timu nyingine na kukiri kuwepo na mazungumzo lakini hakuweka wazi kama tayari amesaini mkataba wa awali na wakali hao wa Afrika Kusini au timu nyingine tofauti na Yanga.

Gamondi alisema kwa kuwa kazi yake ni ukocha basi anaweza kufundisha timu na baadae kuondoka kwenda sehemu nyingine anayoona anaweza kufanya nayo kazi hivyo hajui msimu ujao atakuwa akiifundisha timu gani.

“Makocha tunaajiriwa na kufukuzwa, kama nikiondoka hapa (Yanga) naamini nitapata timu nyingine na nitafanya vizuri na kufukuzwa pia, bila kujali nimeondoka vipi,” alisema Gamondi.

UONGOZI WA YANGA UNAPAMBANA KUMBAKIZA

Licha ya kwamba mawazo ya kocha huyo ni kuondoka Yanga msimu huu, lakini bado viongozi wa timu hiyo wanaendelea kupambana kuhakikisha wanampa mkataba mpya.

Moja ya vigogo wa timu hiyo jina lake linahifadhiwa alisema bado Yanga haijakata tamaa kuhusu kumbakisha kocha huyo lakini ni jambo ambalo linazidi kuwa gumu.

“Yanga ina mpango na Gamondi. Tulimuita na kuongea naye kuhusu mkataba mpya mapema tu lakini alituambia tumpe muda ili amalize msimu kisha tutazungumza.

“Tunajua kuna timu zimempa ofa nzuri ila tunapambana nazo kuhakikisha tunashinda vita hii,” alisema kiongozi huyo.

Aidha kitu kinachompa ugumu kocha huyo kuongeza mkataba ndani ya Yanga ikiwemo vipengele alivyowekewa kwenye mkataba mpya.

Inaelezwa miongoni mwa malengo ambayo kama Gamondi atasaini mkataba mpya ndani ya Yanga atatakiwa kuyatimiza ni pamoja na kuifikisha timu hiyo nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika sambamba na kutetea mataji yote ya ndani ikiwemo lile la ligi. Gamondi anataka kujiweka pembeni katika presha hiyo huku akiamini anahitaji changamoto mpya nje ya Yanga.

Jana Jumatano, Yanga na Gamondi walitarajiwa kukutana katika kikao cha mwisho ambacho kitaamua hatma ya kocha huyo kama ni kusalia Jangwani ama kuondoka.

SOMA NA HII  IMBA, YANGA WAWEKA MIPANGO YAO HII HADHARANI