Home Uncategorized LIVERPOOL YAINGIA VITA NA MANCHESTER UNITED KUPATA SAINI YA ADAMA

LIVERPOOL YAINGIA VITA NA MANCHESTER UNITED KUPATA SAINI YA ADAMA

IMEELEZWA kuwa Liverpool imeingia vitani na Klabu ya Manchester United kuitafuta saini ya winga mwili jumba, Adama Traore anayekipiga ndani ya Wolves.
Vinara hao wa Ligi Kuu England chini ya Kocha Mkuu, Jurgen Klopp wakiwa na pointi 82, tayari wameanza kufanya mpango wa kukaa mezani na mabosi wa Wolves ili wapate saini ya winga huyo ambaye ni chaguo la kocha wa Liverpool.
Kikwazo kikubwa kuipata saini ya nyota huyo inatajwa kuwa itakuwa ni Manchester United ambao nao wanaitaka saini ya winga huyo baada ya kuwa kwenye mwelekeo wa kuikosa saini ya mshambuliaji Timo Werner ambaye yupo njiani kutua ndani ya Klabu ya Chelsea.
Kocha Mkuu wa Woves, Nuno Espirito bado anafikiria kumpata mbadala wa nyota huyo ikiwa ataondoka kwa kuwa amekuwa na mchango mkubwa ndani ya klabu hiyo msimu huu.
Ametupia jumla ya mabao sita na kutoa pasi 10 zilizoleta mabao ndani ya Klabu ya Wolves iliyo nafasi ya sita na pointi zake 43 kibindoni.
SOMA NA HII  ORODHA YA MAJINA YA WANAOWANIA TUZO ZA VPL,2019/20