Home Uncategorized JEMBE HILI LA KAZI SIMBA KUTUA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA

JEMBE HILI LA KAZI SIMBA KUTUA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA

JEMBE la kazi ndani ya Klabu ya Simba, Clatous Chama anatarajiwa kutua Bongo muda wowote kuanzia sasa akitokea nchini Zambia.

Chama alisepa Bongo baada ya Serikali kusitisha masuala ya michezo Machi 17 kutokana na kuibuka janga la Corona ambalo linaivurugavuruga dunia.

Kwa sasa Serikali imeruhusu masuala ya michezo kuanza kwa kueleza kuwa hali ya maambukizi imepungua huku ikiwasisitiza wadau wa michezo kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona. 

Sven Vandenbroeck,  Kocha Mkuu wa Simba alisema kuwa Chama anaweza kurejea nchini kati ya Juni 7/8 kuungana na wenzake ambao walianza mazoezi Mei 27.

Chama ametupia mabao mawili na kutoa pasi saba za mabao kati ya mabao 63 ya Simba.

SOMA NA HII  MAJEMBE HAYA MANNE YA KIMATAIFA YAKUBALI KUTUA YANGA MAZIMA, GSM WAWEKA NENO