Home Tetesi za usajili NYOTA WA SIMBA KUIBUKIA NAMUNGO FC

NYOTA WA SIMBA KUIBUKIA NAMUNGO FC

 KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Miraj Athuman inaelezwa kuwa yupo kwenye hesabu za kutua ndani ya Namungo FC ya Lindi.

Nyota huyo mzawa kwa msimj wa 2020/21 hajawa katika ubora wake ndani ya Ligi Kuu Bara kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara pamoja na ushindani wa namba.

Kwa nafasi ambayo anacheza ndani ya Simba inayonolewa na Didier Gomes ni Luis Miquissone na Clatous Chama walikuwa wakitumika mara kwa mara.

Habari zinaeleza kuwa nyota huyo hajaongezewa mkataba mpya kwa kuwa dili lake la miaka miwili alilosaini akitokea Lipuli limemeguka.

“Sheva bado hajaongezewa mkataba na bado hajazungumza na mabosi wa Simba hivyo inawezekana akaondoka Simba ama akabaki kutokana na maamuzi ya mwalimu,” ilieleza taarifa hiyo.

Kuhusu suala hilo hivi karibuni meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu alisema kuwa ikifika wakati kila kitu kitawekwa wazi.

Ofisa Habari wa Namungo,  Kidamba Namlia alisema kuwa masuala ya usajili anayesimamia ni Katibu Mkuu wa Namungo hivyo hawezi zungumzia suala la Sheva.

SOMA NA HII  WAKATI YANGA WAKIWA KWENYE NAFASI YA KUMPATA MPOLE...SIMBA WAPANGA KUPINDUA MEZA KIBABE ...'WAANZA FUJO'....