Home Habari za michezo FEI TOTO CHANZO CHA BANGALA KUCHEZESHWA BEKI…NABI AFUNGA KESI KWA KUMKABIDHI...

FEI TOTO CHANZO CHA BANGALA KUCHEZESHWA BEKI…NABI AFUNGA KESI KWA KUMKABIDHI RASMI MAJUKUMU MAPYA…


Mashabiki wa Yanga wamezoea kuona beki wao wa kati Mkongomani Yannick Bangala akicheza kiungo mkabaji lakini kocha wao Nasreddine Nabi amewaambia watulie vinginevyo pale kwa kina Feitoto hapatakalika.

Nabi amesema kuwa ameona mijadala ya mashabiki juu ya kutaka Bangala arudishwe kucheza kama kiungo na kwamba amekuwa na maoni tofauti.

Kocha huyo mwenye misimamo aliongeza kuwa hatua ya kumrudisha Bangala kucheza nafasi ya beki pia ni kutoa nafasi kwa viungo wengine kuanza hasa wazawa akiwemo Feisal Salum ambaye ameonyesha kuimarika zaidi.

“Ukimchezesha Bangala kwenye kiungo wakati huu tuna Aziz KI unapunguza nafasi ya wengine kucheza, tunahitaji nguvu ya Feisal nafikiri watu hawaangalii ubora wa Feisal anavyocheza sambamba na Azizi KI na Mayele, ”alisema Nabi.

“Mimi namjua Bangala tangu nikiwa DC Motema Pembe, huyu ni beki halisi na hapo anapocheza sasa ni sehemu yake halisi ambayo imemtambulisha, mimi ndiyo nimemleta hapa huyu pamoja na Mayele (Fiston) kwa kuwa nawajua sio kuanzia hapa Tanzania.

“Sina tatizo kama Bangala akicheza kama kiungo nakubaliana nao anajua kucheza vizuri pia eneo hilo na maeneo mengine hii inatokana na ubora wake mkubwa.”

Msimu huu Bangala amekuwa akiwabadili mabeki Bakari Mwamnyeto na Dickson Job katika nani acheze na mchezaji bora huyo wa ligi msimu uliopita ingawa Yanga imesharuhusu mabao matatu katika mechi zao nne za ligi.

SOMA NA HII  AL HILAL YAIBAMIZA MABAO 2-1 TP MAZEMBE, SIMBA SUPER CUP