Home Habari za michezo SIMBA WAPIGA BAO LA KISIGINO….MASHINE YA KAZI YATUA….MSHAHARA WAKE NI KUFRU TUPU…

SIMBA WAPIGA BAO LA KISIGINO….MASHINE YA KAZI YATUA….MSHAHARA WAKE NI KUFRU TUPU…

Habari za Simba leo

UONGOZI wa Simba umemtambulisha kiungo mkabaji rai wa Senegal,  Babacar Sarr kwa mkataba wa miaka miwili kujiunga na kikosi cha Wekundu hao wa Msimbazi kipindi hiki cha dirisha dogo.

Kiungo huyo mwenye uzoefu wa kucheza soka la Afrika ambapo mbali na US Monistir aliwahi kucheza katika klabu mbalimbali ikiwemo Olympique  Beja ya Tunisia,  Teungueth FC. Aspikine na Mbour P.C.

Sarr anauwezo mkubwa wa kucheza kama kiungo mkabaji wakati mwingine anauwezo wa kucheza kama kiungo mshahara anakuja kuungana na viungo wengine akiwemo Fabrice Ngoma,  Sadio Kanoute, Mzamiru Yassin na Abdallah Hamis.

Tetesi za Usajili SimbaTaarifa kutoka ndani ya Simba zinadai kuwa Sarr , atakuwa kilipwa mshahara wa dola 6000 sawa na zaidi ya Milioni 15 za kitanzania, pia atapewa Nyumba ya kuishi ya kisasa, gari na mahitaji mengine ya kistaa.

Kiungo huyo anakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa kipindi cha dirisha dogo la usajili baada ya koungo Salehe Karabaka aliyesajiliwa kutoka JKU FC ya Visiwani Zanzibar wiki iliyopita.

Kwa mujibu wa Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba,  Ahmed Ally kuwa bado usajili unaendelea na vifaa vinaendelea kuleta kuhakikisha wanaimarisha timu hiyo kulingana na mahitaji ya kocha.

Kuhusu Michael Charamba aliyeonekana jana katika mchezo wa kombe la Mapinduzi kati ya Simba na APR, Ahmed alisema yuko katika majaribio na suala lote la usajili lipo mikononi mwa kocha Abdelhak Benchikha.

“Usajili bado tunaendelea na kuna wachezaji wengi tunatarajia kuwatambulisha. Kuhusu Charamba yupo kwenye majaribio na muamuzi ya kusajili yatabaki wa kocha ambaye anajukumu hilo, ” amesema Ahmed

SOMA NA HII  KADUGUDA: - 'KAMA INAHITAJIKA MTU AFE ILI TUWE MABINGWA ..NIPO TAYARI...NITAFUNGUA TAWI AKHERA...'