Home Habari za michezo ANAYEFUATA KUTAMBULISHWA SIMBA HUYU HAPA….TAYARI YUKO ZAKE ZNZ MAPEMA TU…

ANAYEFUATA KUTAMBULISHWA SIMBA HUYU HAPA….TAYARI YUKO ZAKE ZNZ MAPEMA TU…

Tetesi za Usajili Simba SC

Simba wakati wowote kutoka sasa itamtangaza winga wao mpya Ladack Chasambi ambaye tayari yupo kisiwani hapa tayari kwa utambulisho huo.

Chasambi anayesajiliwa na Simba akitokea Mtibwa Sugar ya Morogoro amewasili hapa Unguja jana kwa usiri mkubwa baada ya kuachwa kwenye msafara wa kikosi cha Taifa Stars kilichokwenda kwenye Fainali za Mataifa Afrika zinazofanyika kule Ivory Coast.

Simba ilishamalizana na Mtibwa Sugar juu ya usajili wa Chasambi lakini pia mchezaji mwenyewe na kupewa baraka zote za kujiunga na wekundu hao.

Simba leo imeanza mchakato wa kumfanyia utambulisho huo Chasambi ambaye anakwenda kujibu maombi ya kocha wao Abdelhak Benchikha aliyetaka kuletewa winga wa kulia.

Inaelezwa pia kwenye dili hilo la Chasambi pia wekundu hao watamfungulia milango kiungo wao kiraka Nassoro Kapama ambaye yupo kwenye adhabu ya kusimamishwa na wekundu hao.

Mbali na Chasambi pia Simba imeshamalizana na winga wa kushoto Edwin Balua ambapo sasa kilichosalia ni wekundu hao kumalizana na klabu yake ya Prisons ya Mbeya.

SOMA NA HII  KUHUSU CHAMA NA KUONGEZA MKATABA SIMBA...UKWELI UNAOPASWA KUJUA HUU HAPA...