Home news SIMBA WATOA MILIONI 10 HOSPITALI YA MWANANYAMALA

SIMBA WATOA MILIONI 10 HOSPITALI YA MWANANYAMALA

 


UONGOZI wa Klabu ya Simba leo Septemba 15 umetoa kiasi cha Sh milioni 10 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala kwa ajili ya kusaidia afya ya mama na mtoto.

Kwa sasa Klabu ya Simba ipo kwenye Wiki ya Simba ambayo ilianza Septemba 13 na inatarajiwa kukamilika Septemba 19.

Muda huu mambo ambayo wanayafanya ni matendo ya huruma kwa jamii pamoja na kufanya usafi katika maeneo mbalimbali Tanzania.

Muongoza msafara alikuwa ni Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba, Barbra Gonzale aliongozana pamoja na viongozi wengine na mashabiki pia.

Septemba 19, Uwanja wa Mkapa kunatarajiwa kuwa na mchezo wa kirafiki kati ya Simba na TP Mazembe ambao unatarajiwa kuwatambulisha wachezaji wote wa Simba kwa msimu wa 2021/22.

SOMA NA HII  TAJIRI TAJIRI TU...HIVI NDIVYO GSM ALIVYOZIMA ISHU YA NABI KUFUKUZWA YANGA...MAMBO HAYA 5 YALIKUWA LAZIMA 'ASEPE'...