Home Ligi Kuu MTIBWA SUGAR YAPANIA KUTEMBEZA DOZI

MTIBWA SUGAR YAPANIA KUTEMBEZA DOZI


 UONGOZI wa Mtibwa Sugar umeweka wazi kwamba utatembeza dozi kwenye mechi zilizobaki ili kupata pointi zitakazowapa nafasi ya kubaki ndani ya ligi.

Ikiwa imecheza jumla ya mechi 32 na pointi zake ni 38 haina uhakika wa kubaki kwenye ligi ikiwa itapoteza mechi zake zote mbili kwa kuwa pointi hizo zinaweza kufikiwa na Ihefu yenye pointi 35 ikiwa ipo nafasi ya 15.

 Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa wanatambua ushindani ni mkubwa ila watapambana kutembeza dozi ili wapate ushindi.

“Mechi ambazo zimebaki tutapambana kupata ushindi kwa kutembeza dozi, inawezekana na kila timu inahitaji kufanya vizuri hivyo ni suala la kusubiri pale tutakapokuwa uwanjani, mashabiki watupe sapoti.

“Mbinu ambazo wachezaji wanapata pamoja na utayari wao wa kufanya vizuri ni jambo ambalo linaongeza nguvu kwa wachezaji kupambana ili kupata matokeo chanya,” .

Mchezo wao ujao wa Mtibwa Sugar ni dhidi ya Dodoma Jiji iliyo nafasi ya 9 na pointi 42 Uwanja wa Jamhuri, Dodoma itakuwa Julai 15.

SOMA NA HII  MSIMAMO WA LIGI KUU TANZANIA BARA