Home Habari za michezo MANGUNGU ATOA KAULI YA KIBABE LEO SIMBA DHIDI YA POWER DYNAMO

MANGUNGU ATOA KAULI YA KIBABE LEO SIMBA DHIDI YA POWER DYNAMO

Habari za Simba

Mwenyekiti wa Simba SC, ametoa kauli ya kibabe kuelekea mchezo wao dhidi ya Power Dynamod majira ya saa 10 jioni hii leo Septemba 16, 2023.

“Simba ni timu kubwa kama inavyofahamika na watu wenye uelewa wa soka, hatuogopi kucheza na timu yoyote tumeshazifunga timu nyingi za Afrika Magharibi, Afrika ya Kaskazini na sasa tupo hapa Zambia kucheza na tutacheza na Power Dynamos ambao tulichezanao mechi ya kirafiki kwenye Simba Day.

Inaweza kuwa mechi ngumu kwa sababu tunacheza dhidi ya timu ambayo tumechezanayo katika kipindi kifupi kilichopita, watakuwa wamerekebisha makosa yaliyopelekea sisi tukashinda lakini naamini benchi letu la ufundi litakuja na mbinu za kuhakikisha tunashinda mechi hiyo,” alisema Mangungu

SOMA NA HII  AL AHLY WAIPIGA MKWARA MZITO YANGA,GAMONDI APEWA TAMKO HILI