Home Habari za michezo AHMED ALLY:- SERIKALI HAIJAFANYA SAWA…SISI MASHABIKI WAMEJILIPIA MIL 3 KWENDA MISRI…

AHMED ALLY:- SERIKALI HAIJAFANYA SAWA…SISI MASHABIKI WAMEJILIPIA MIL 3 KWENDA MISRI…

Habari za Simba leo

Anaandika Meneja wa idara ya habari na mawasiliano wa klabu ya Simba Ahmed Ally kupitia Instagram yake; ——— Baadhi ya Mashabiki wa Simba waliojilipia nauli zao kusafiri kwenda kuipa support timu yao Nchini Misri

Kila shabiki amejilipia Dola 1200 sawa na Milioni 3,126,000

Hili swala la Serikali kusafirisha Mashabiki nitatoa maoni yangu nikimalizana na Al Ahly, Sasa hivi akili inawaza namna ya kufuzu Nusu Fainali, Ila msimamo wangu ni kwamba si jambo jema hata kidogo

Kwa Mashabiki mpira ni starehe hivyo Serikali haiwezi kugharamia watu kwenda kustarehe.

Tena bora ingekua imetoa usafiri tu. Lakini wametoa Posho Dola 500 kila kichwa sawa na Milioni 1,200,000 kwa ufupi hawa Mashabiki wamenuniliwa na wanalipwa kuishangilia timu yao

Na hao sio Mashabiki wa kawaida ni Machawa wanaotetea maslahi ya viongozi wao yaani Serikali imelipia Machawa wa watu

Kuwalipia nauli sio kuwapenda ni kufuga tatizo ambalo baadae hatutaweza kulitatua

Leo unalipia mashabiki wa klabu, kesho Ali Kiba ataiomba Serikali iwagharamie mashabiki wake kwenda Marekani kufanya show utamnyima??

Twaha Kiduku ataomba aende kupigana Uingereza na mashabiki wake utamnyima??

Halafu nyie Nyuma Mwiko acheni kuzuga huwezi kulipia nauli watu 48 ukajidai eti unawapenda mashabiki zenu, Wakati kwenye mechi yenu juzi Mashabiki wameumia, wamepigwa mabomu ya machozi, watu wamepata vilema, na hamjasema chochote halafu uje uzuge eti unawapenda watu wenu

Ndugu zangu wana Simba hili swala lisiwatie unyonge na wala Serikali yetu haina nia ya kufanya ubaguzi

Sisi tuendelee na utamaduni wetu kujisimamia tukipata msaada tutachukua lakini katu tusilemae kusubiri dezo

We are Simba Sisi ni Wakubwa, Sisi ni Wafalme, Sisi tuna hadhi kubwa

Lets focus na mechi yetu ya Ijumaa

SOMA NA HII  GOMES.., ADEL NA MILTONI WAKOSEKANA MAZOEZI YA SIMBA...HATMA ZAO KUJULIKANA LEO