Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI YA MAMELOD vs YANGA….TIKETI KUUZWA LAKI 4 ZA KIBONGO…UTARATIBU HUU...

KUELEKEA MECHI YA MAMELOD vs YANGA….TIKETI KUUZWA LAKI 4 ZA KIBONGO…UTARATIBU HUU HAPA

Habari za Michezo

Mbali na gharama za tiketi kwenye sehemu za mzunguko kutangazwa kuwa ni Tsh 3,000 tiketi za maeneo mengine zinafika hadi Tsh Laki nne eneo la VIP ila nimevutiwa sana na utaratibu wa ukataji tiketi pamoja na maelekezo mengine ya kuingia uwanjani ambayo kimsingi ni vizuri kama Taifa tukaanzia hapa kwa kujifunza na kwa watanzania wanaokuja wajue pia utaratibu ulivyo.

1. Watoto wanatakiwa kukatiwa tiketi kama ilivyo kwa watu wazima hapo wamewaondoa kundi la watoto walio chini ya miezi 18 ambao hao wana utaratibu maalumu lakini ni lazima uwe na cheti cha kuzaliwa.

Kwa masharti haya ni wazi wanatengeneza mazingira ya usalama kwa sababu muda mwingine viwanjani sio sehemu salama sana hivyo watoto hawatakiwi na kama atakuja masharti ndio hayo na mwisho Klabu haihusiki kwa chochote.

2. Watu wenye changamoto ya ulemavu wao pia wana eneo lao maalumu la kukaa, lakini sio kwenda tu kuna maeneo maalumu ya kujiandikisha kimtandao ili kuwa na idadi maalumu kabla ya siku ya mchezo, hapa pia Klabu haitahusika ilitokea upotevu wala kifo cha shabiki

3.Eneo lingine lililotolewa angalizo kwenye vyanzo rasmi vya Klabu ni watu kuepuka tiketi za mtu kati au kununulia uwanjani, mwisho wameitaja njia sahihi ya kununua tiketi kwa watu online! Mzigo ukikata umekata

MASHARTI MENGINE Tiketi hairudishwi, usije na chochote ambacho kinaweza kutumika kama silaha, Redio haziruhusiwi uwanjani, ni Lazima kuzingatia mipaka ya utulivu na kuwa na adabu ukiwa uwanjani, usivute sigara au chochote ukiwa uwanjani na sehemu ya kukaa ni pale tiketi inapokuelekeza kila mtu atakaa panapo muhusu.

Angalizo lingine muhimu ambalo wamesisitiza sana, kwa kuwa umekata tiketi kwa hiyali yako chochote kitakachotokea Klabu haihusiki, majeraha, upotevu wa mali na hata vifoni juu ya mtu binafsi kuwa muangalifu ila sio kuihusisha Klabu.

SOMA NA HII  ENDORPHINE FAIRYTALE -SHANGWE LA SLOTI DISEMBA HII! CHEZA NA UJISHINDIE ZAWADI KABAMBE ZA FEDHA...!