Home Habari za michezo MASTAA SIMBA KUMWAGIWA MIL 812 KUZITOA MAMELOD NA AL AHLY….MABOSI WACHARUKA…

MASTAA SIMBA KUMWAGIWA MIL 812 KUZITOA MAMELOD NA AL AHLY….MABOSI WACHARUKA…

Habari za Michezo leo

Ikiwa imesalia siku moja tu kabla ya mechi za marudiano za hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kuchezwa, mkwanja mrefu umeweka mezani kama hamasa kwa wachezaji wa Simba na Yanga.

Iko hivi; Simba wameahidiwa Sh512 milioni endapo watapata ushindi na kuing’oa Al Ahly huko Cairo, Misri huku wakiwa na kibarua kigumu kwani walishafungwa 1-0 nyumbani.

Yanga nao wamewekewa mezani Sh300 milioni endapo wataweza kuwang’oa Masandawana huku wakiwa na kazi ya ziada ya kufunga ugenini kwani nyumbani walishapaki basi walipotoka suluhu.

Bila kusahau, Rais Samia Suluhu Hassan tayari alishaahidi kununua kila bao la ushindi kwa Sh10 milioni katika mechi hizo.

Unaweza kusema vigogo hawa wawili wamebaki na dakika 90 tu, tena ugenini ili kuthibitisha kuwa wanachukua au wanauacha mzigo huo mzito waliowekewa mezani.

Ikumbukwe kuwa wikiendi ilimalizika, huku Watani wa jadi wakicheza mechi ngumu za kimataifa na wote walikuwa nyumbani katika uwanja wa Benjamin Mkapa.

Simba walitawala mchezo kwa takwimu zote na kila mmoja anaamini walistahili kuwafunga mabingwa hao mara 11 wa Afrika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Ijumaa iliyopita, lakini kinyume chake Wekundu wakalala 1-0.

Kwa kuangalia mechi iliyopita ya jijini Cairo iliyopigwa Oktoba 24, 2023 baina ya timu hizo ambayo ilimalizika kwa sare ya 1-1, ni Simba ndiyo iliyotangulia kufunga bao kabla ya wenyeji kusawazisha, jambo linaloleta picha kuwa Wekundu wa Msimbazi wanaweza kufunga hata ugenini dhidi ya Ahly, hivyo nguvu ikiongezwa wanaweza kutoboa.

Baada ya kucheza kwa kujilinda, Yanga walitengeneza nafasi nyingi dhidi ya Masandawana Kwa Mkapa, hiyo ikimaanisha kuwa lango la Mamelodi walioruhusu bao moja tu katika mechi saba za kuanzia makundi hadi robo fainali ya kwanza, wanafikika langoni mwao lakini ni lazima umakini uongezwe ili kuwafunga ikizingatiwa wao pia wamefunga mabao 7 tu katika mechi hizo 7, ikiwa ni wastani wa bao moja kwa kila mechi.

Wote hawa wanakwenda ugenini na safari zao zitaanza leo, huku vichwa vyao vikiwaza jambo moja tu kubwa, kuwang’oa wapinzani wao na kutinga nusu fainali. Na bila ya maswali, kuvuta mkwanja waliowekewa maezani.

SOMA NA HII  BALAA JIPYA YANGA HILI HAPA...KAZE AFUNGUKA KILA KITU...MAYELE , 'FEI TOTO' WATAJWA...