Home Habari za michezo AL AHLY WAIPIGA MKWARA MZITO YANGA,GAMONDI APEWA TAMKO HILI

AL AHLY WAIPIGA MKWARA MZITO YANGA,GAMONDI APEWA TAMKO HILI

Habari za Michezo

Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Soka Barani Afrika Al Ahly Marcel Koller ameliambia amesema kikosi chake kipo tayari kwa mchezo wa kesho Jumamosi (Desemba 02), huku wakitarajia kucheza kwa nidhamu kubwa dhidi ya Young Africans.

Kocha huyo kutoka nchini Uswiz amesema wanatambua watachez ana timu yenye uwezo na ubora mkubwa, hivyo wanakuja Tanzania wakiwa wamejipanga kwa kutumia mikakati itakayowafanya kucheza kwa tahadhari ndani ya dakika 90.

“Tutajaribu kuonyesha kilichokuwa bora kwa ajili ya kupata matokeo mazuri, Young Africans ni timu yenye wachezaji wazuri wenye uwezo mkubwa kwa sababu tulipata nafasi va kuifuatilia katika mchezo wao walipocheza dhidi ya CR Belouizdad hivyo ni lazima tujipange sana.” Amesema Koller

Kikosi cha Al Ahly kiliwasili jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia leo Ijumaa (Desemba Mosi), tayari kwa mchezo wa Mzunguuko wa Pili wa Kundi D, Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Timu hizo zilizopo Kundi D zinakutana katika mchezo huo utakaopigwa majira ya saa l:00 usiku kwa saa za Afrika mashariki, huku Al Ahly ikitoka suluhu katika mechi iliyopita ya Ligi Kuu ya Misri dhidi ya Smouha na kufikisha pointi 14 nyuma ya vinara Pyramids wenye pointi l6.

Young Africans inahitaji ushindi ili kufufua matumaini ya kutimiza ndoto zao za kwenda Robo Fainali kupitia kundi hilo kwani baada ya hapo itakwenda nchini Ghana kukiputa dhidi ya Medeama.

SOMA NA HII  PIGA MSHINDO WA UHAKIKA UKIWA NA ODDS HIZI ZA USHINDI KUTOKA MERIDIANBET...