Home Habari za michezo ALLY KAMWE:- TUMETOKA LAKINI TUNA REKODI ZETU….ANAYESEMA TUMEKIMBIA AJE TUKIPIGE..

ALLY KAMWE:- TUMETOKA LAKINI TUNA REKODI ZETU….ANAYESEMA TUMEKIMBIA AJE TUKIPIGE..

Habari za Yanga

Wakati mashabiki wa Simba wakitamba kwamba watani wao Yanga wamewakimbia kwa kukubali kipigo mbele ya APR wamejibiwa wakiambiwa leteni barua ya kuomba mechi tukipige.

Meneja Habari na Mawasiliano Yanga, Ally Kamwe amesema klabu yao imeyapokea matokeo iliyopata jana dhidi ya APR lakini hakuna ukweli kwamba wameikimbia timu yoyote kwani hakuna wanayemuogopa.

Yanga jana imepokea kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa APR kwenye mechi ya robo fainali ya Kombe la Mapinduzi iliyopigwa Uwanja wa New Amani Complex hapa Unguja.

Kamwe amesema Yanga inatoka ikiwa na timu yenye rekodi ya kutoa kipigo kikubwa ambacho kimekuwa maaarufu kukitoa kwa klabu mbalimbali.

Amesema kama kuna timu inaona imekimbiwa waiandikie barua mapema waombe kucheza nao kabla ya wao kuondoka Unguja kisha waonyeshane ubabe.

“Yanga inawezaje kuogopa hizi timu zingine hasa Yanga hii ya msimu huu? Mashabiki wetu watulie tumepoteza mchezo kihalali dhidi ya APR makocha wetu wamepata nafasi ya kuchukua changamoto hizo na kwenda kuzifanyia kazi na sisi tuliobaki tunapaswa kuwaachia wao,” amesema Kamwe

“Kama wapo ambao wanaona tumewakimbia basi watuandikie barua watuletee haraka kabla hatujaamua safari ya kurudi kwetu, tuonyeshane, sisi ndio timu ambayo imetoa kipigo kikubwa hapa, tena kile ambacho tuliwapiga wale jamaa,”

SOMA NA HII  SIMBA YATAJA SIRI ...MWARABU ANAKUFA DAR..MORRISON KUPANGUA KIKAOSI...MHILU AFUNGUKA MAPYA ...

1 COMMENT