Home Habari za michezo MCHAMBUZI;- MASTAA HAWA NDIO WAMEIANGUSHA YANGA JANA…WALISTAHILI KUFUNGWA 5..

MCHAMBUZI;- MASTAA HAWA NDIO WAMEIANGUSHA YANGA JANA…WALISTAHILI KUFUNGWA 5..

Habari za Yanga leo

Kwenye mchezo dhidi ya Jamhuri ,Yanga walicheza kawaida ila walikutana na timu ya kawaida wakaifunga magoli matano,mchezo dhidi ya Jamus walipata shida kupata ushindi na ushindi ulikuja dakika za lala salama

Jana dhidi ya APR ilikuwa moja kati ya mechi nzuri na wamefungwa magoli matatu .

Kipindi cha kwanza Yanga walitawala na waliona game kama rahisi ,back pass zilikuwa nyingi hata sehemu ambazo hazikuwa na ulazima

Goli la kusawazisha la APR ndio liliwarudhisha mchezoni na kama wangekuwa na utulivu zaidi ule mnara wa 5G ungesimama jana

Msheri alikuwa nje muda mrefu hajacheza lakini kiwango alichoonesha anaonekana kabisa huyu ana kitu,Naanguka pia alikuwa na game nzuri sana na mwingine ni Shekhani hata alivyoingia aliongeza kitu

Wachezaji hawa wamepewa nafasi na wameonesha wanakitu,Yanga itaangalia inawatumiaje

Lakini kuna wachezaji wazoefu kama Ngushi ,Mauya na Mkude wameiangusha Yanga kwa kweli

Ukiacha magoli mawili aliyofunga mechi ya kwanza ,mechi zingine ameonesha kwanini anakaa nje na Mashabiki wamepata majibu kwanini hawa wanakaa nje

Master Tindwa via HiliGame ya CloudsFM

SOMA NA HII  PAMOJA NA YANGA KUINGIA ROBO FAINAL CAF....ALLY KAMWE AANIKA TIMU WANAYOIHOFIA KUKUTANA NAYO...