Home Habari za Yanga Leo MUDATHIR ATUNUKIWA TUZO… MVP…AUCHO & MUSONDA WAHUSIKA

MUDATHIR ATUNUKIWA TUZO… MVP…AUCHO & MUSONDA WAHUSIKA

Habari za Yanga leo

MUDATHIR YAHYA, Mzee wa Simu ziishe amaumaliza msimu wa 2023/24 kwa aina yake nzuri ya ushangiliaji ambayo ilikuwa gumzo kwa mashabiki na wapenzi wa soka, lakini licha ya hayo pia amechaguliwa kuwa mchezaji bora (MVP)kwa upande wa wachezaji wa Yanga.

Tuzo za Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) msimu wa 2023/24 zitatolewa wakati wa mchezo wa Ngao ya Jamii tofauti na awali zilipokuwa zinafanyika siku tatu kabla ya kumalizika kwa fainali ya Kombe la Shirikisho.

Lakini kabla ya tuzo hizo kutolewa, nyota wa Yanga, Khalid Aucho na Kennedy Musonda kwenye ukurasa wa Mudathir Yahya wamemtunuku tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka (MVP).

Kupitia Instagram ya Mudathir aliweka picha akiwa na wawili hao baada ya kuchukua kombe la pili msimu huu baada ya kuchukua la Ligi Kuu na ndipo Aucho aliandika;

“Familia mchezaji wangu bora wa msimu, endelea kufanya kile unachofanya vyema zaidi ya msimu huu.” Kwa upande wa Musonda aliandika;

“Familia kwangu umekuwa mchezaji wangu bora na thabiti zaidi msimu huu kaka endelea kupambana.”

Mudathir alimaliza msimu na mabao tisa akiwa kwenye 10 bora ya vinara wa mabao wa Ligi Kuu, ambapo Stephane Aziz KI anayekipiga pia katika timu hiyo akibeba kiatu cha dhahabu baada ya kupachika mabaoi 21 katika Ligi Kuu Bara.

Wakati huo Clement Mzize akichukua  kiatu cha ufungaji bora wa Kombe la Shirikisho akifunga mabao matano sawa na Edward Songo wa JKT Tanzania

SOMA NA HII  WAKATI SIMBA WAKIPANGA KUMUAGA MKUDE....MANARA KAIBUKA NA HILI JIPYA...AMETAJA MO DEWJI TENA...