Home Uncategorized LAMINE AIPA YANGA HASARA NYINGINE

LAMINE AIPA YANGA HASARA NYINGINE

YANGA imemkata beki wao, Lamine Moro Sh.1 milioni kwenye mshahara wake kwa kitendo kisicho cha kiungwana alichomfanyia Mwinyi Kazimoto lakini kikanuni bado atawapa hasara.

Mchezaji huyo raia wa Ghana, alionyeshwa kadi nyekundu juzi kwenye mechi dhidi ya JKT Tanzania mjini Dodoma kwa kumkanyaga mgongoni kiungo Mwinyi Kazimoto.

Tukio la Lamime kikanuni litaipa hasara Yanga kwani atalazimika kukosa mechi tatu muhimu za Ligi dhidi kati ya tisa zilizobaki.

Yanga kwanza itamkosa dhidi ya Azam Jumapili hii ikifuatiwa na Namungo na ile ya Ndanda zote zikipigwa Dar es Salaam.

Mchezaji huyo ambaye amekuwa chaguo la Kocha Luc Eymael kutokana na ubora wake, sasa atalilazimisha benchi la ufundi kuwatumia wazawa Kelvin Yondani, Juma Makapu na Andrew Vincent Dante kwa nyakati tofauti.

Luc amekiri kwamba kitendo alichofanya mchezaji huyo si cha kiungwana lakini amemuombea radhi kwa madai kwamba si mnyama kiasi hicho bali alighafilika.

SOMA NA HII  MASAU BWIRE AJA NA KUPAPASA NA KUKUNG'UTA