Home Uncategorized KIBAYA WA MTIBWA SUGAR ATAJA ATAKAPOKUWA MSIMU UJAO

KIBAYA WA MTIBWA SUGAR ATAJA ATAKAPOKUWA MSIMU UJAO


JAFFARY Kibaya, mshambuliaji wa Mtibwa Sugar amesema kuwa ataendelea kubaki ndani ya klabu hiyo msimu ujao kutokana na kufurahia maisha anayoishi hapo alipo kwa sasa.

Imekuwa ikielezwa kuwa Simba na Yanga zinaiwinda saini ya mshambuliaji huyo mzawa anayefanya vizuri ndani ya uwanja.

Kibaya amesema:”Maisha yangu ndani ya Mtibwa Sugar ni mazuri na kila kitu ninachohitaji ninakipata hivyo sifikirii kusepa kwa sasa.”.

Mtibwa Sugar yenye ngome yake mkoani Morogoro ipo chini ya Kocha Mkuu Zuber Katwila ikiwa nafasi ya 14 kibindoni ina pointi 33.

SOMA NA HII  ISHU NZIMA YA USAJILI YANGA ILIPOFIKIA, MIPANGO KABAMBE YAANIKWA - VIDEO