Home Uncategorized WAWILI WANAOWINDWA NA SIMBA KUTIMKIA MOROCCO

WAWILI WANAOWINDWA NA SIMBA KUTIMKIA MOROCCO


UONGOZI wa Mtibwa Sugar umesema kuwa kwa sasa wanafikiria kuwapeleka nje ya nchi nyota zao wawili ambao ni Kibwana Shomari na Dickson Job ambao ni mabeki wanaowindwa na Simba.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa mpango wao mkubwa kwa sasa ni kuwapeleka nyota wao nje ya nchi ili wakaongeze ujuzi.
“Huyu Job na Kibwana wanawindwa sana hapa Bongo ila sisi tunaona kwamba bado muda wao wa kucheza klabu hizi zenye presha kama Simba na Yanga, tunataka kuwapeleka nje ya nchi ikiwezekana Morroco wakaungane na Simon Msuva ndani ya El Jadida.
“Itawasaidia wao kukomaa na kuwa na uwezo wa kuamua kwani kuna wengi ambao tuliwapeleka hizi timu kubwa walishindwa kufanya vizuri mwisho wa siku wakarudi tena Mtibwa hivyo tuna mipango nao mikubwa,” amesema.
Inaelezwa kuwa Simba inahitaji saini za mabeki hao ili kuongeza nguvu ndani ya kikosi hicho kwa ajili ya kuwa na kikosi kipana.
SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA ALHAMISI