Home Uncategorized FUNDI HUYU WA CONGO KUTUA YANGA, NI YULE ALIYELETWA KININJA NA SIMBA

FUNDI HUYU WA CONGO KUTUA YANGA, NI YULE ALIYELETWA KININJA NA SIMBA


INAELEZWA kuwa uongozi wa Yanga upo kwenye mchakato wa kusaka saini ya kiungo  Fabrice Mugheni, raia wa DR Congo.
Mugheni ni miongoni mwa viungo bora katika Ligi Kuu ya Rwanda na aliwahi kuletwa nchini na aliyekuwa kocha wa Simba, Mrundi, Masoud Djuma lakini viongozi wa timu hiyo hawakuridhishwa na uwezo wake aliouonyesha katika majaribio yake kama ilivyokuwa kwa Mghana, Lamine Moro kabla ya kutua Yanga.
Wakati anatua kwa mara ya kwanza, kiungo huyo mwenye uwezo wa kupiga mashuti ya mbali, alifichwa na viongozi wa Simba ikiwemo kumbadilishia ndege ili kukwepa kuonekana na hata alipotua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), alitolewa kwa usiri mkubwa majira ya saa nane usiku huku akiwa ameziba sura na kukimbizwa haraka kwenye gari iliyokuwa ikimsubiri lakini Championi lilimnasa akipokelewa na Mratibu wa Simba, Abbas Ally.
Taarifa za uhakika kutoka ndani ya Yanga zinasema kuwa tayari Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Kampuni ya GSM, Mhandisi, Hersi Said tayari ameshakamilisha mazungumzo na kiungo huyo na kinachosubiriwa ni kuweza kusaini mkataba tu.
“Unajua usajili wa Sarpong hauwezi kuwa mgumu kwa sababu mkataba wake umevunjwa na Rayon lakini kuna kiungo mwengine yupo pale tayari uongozi unafanya mipango ya kumleta na mchezaji ameonyesha utayari wa kuja kwani mkataba wake unaelekea kuisha.
“Ni yule jamaa mwenye rasta anaitwa Fabrice aliwahi kuja Simba akafanya majaribio lakini wakamkaushia ila mhandisi Hersi ameshamalizana naye na kinachosubiriwa ni hili janga la Corona lipite,” alisema mtoa taarifa.
Championi lilimtafuta kiungo huyo ili aweze kuzungumzia ishu hiyo ambapo alisema: “Ni kweli nimefuatwa na viongozi wa Yanga lakini siwezi kusema nini nimezungumza,”.
SOMA NA HII  MSHAMBULIAJI SIMBA AMALIZANA NA TP MAZEMBE