Home Habari za michezo WAKATI LEO WAKITANGAZA KUANZA ‘MABALAA’….KIGOGO SIMBA AFUNGUKA USAJILI WAO ULIVYO..

WAKATI LEO WAKITANGAZA KUANZA ‘MABALAA’….KIGOGO SIMBA AFUNGUKA USAJILI WAO ULIVYO..

Habari za SImba SC

HUKU wakiendelea na ukarabati mkubwa wa kikosi chao kupitia usajili, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ amewachimba mkwara mzito wapinzani wao msimu ujao, hususani watani zao wa jadi Yanga kwa kuweka wazi kuwa hawatakuwa wanyonge tena na wanasuka kikosi cha mataji.

Simba imekuwa na ukame wa misimu miwili mfululizo bila taji lolote kubwa, huku wakishuhudia mataji hayo yote yakibebwa na watani Yanga hali ambayo imewafanya mashabiki wengi wa Simba kuingia jazba.

Tayari Simba imetangaza kuachana na mchezaji Augustine Okrah na baadhi ya watendaji wa benchi la ufundi, huku leo Jumatatu wakitarajiwa kuendeleza panga lao kwa ajili ya kupata nafasi ya kushusha mashine mpya.

Akizungumzia usajili na mipango yao kuelekea msimu ujao, Try Again alisema: “Nawahakikishia Wanasimba wote kuwa msimu ujao hatutakuwa wanyonge tena, tutakuwa imara kuliko ilivyokuwa awali.

“Tunajua kwa misimu miwili hatukuwa na furaha hususani katika suala la kushinda mataji, lakini msimu ujao tutakuwa bora kwakuwa tutasajili kikosi imara.”

SOMA NA HII  KISA YANGA....MANULA 'AWACHANA LIVE' MASTAA WENZAKE SIMBA...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here