KLABU ya West Armenia imeanza mazungumzo na kinda wa Yanga, Clement Mzize ili kuichezea timu hiyo msimu ujao.
Timu hiyo inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza nchini Armenia inavutiwa na kiwango cha nyota huyo ambaye ameiwezesha Yanga kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC)
Mzize amekuwa kwenye kiwango bora msimu huu akifunga mabao matano ya Ligi Kuu Bara na sita ya ASFC huku akiweza pia kushinda tuzo ya mchezaji bora chini ya miaka 20 katika tuzo za (TFF).
Hivi karibuni mabosi wa klabu hiyo walitiliana saini mkataba wa mashirikiano baina yao na Simba SC, ambapo klabu hizo mbili zitakuwa zikibadilishana wachezaji , makocha, wachezaji vijana na maafisa mbalimbali kwa lengo la kupata uzoefu.