Home Habari za michezo WAKATI TFF WAKIUMA MENO….ZFF WATIA ‘UBANI’ OMBI LA SIMBA KUTUMIA UWANJA WA...

WAKATI TFF WAKIUMA MENO….ZFF WATIA ‘UBANI’ OMBI LA SIMBA KUTUMIA UWANJA WA AMANI..

Habari za Simba leo

Shirikisho la Soka Visiwani Zanzibar ZFF limekiri kupokea barua ya maombi kutoka kwa Klabu ya Wekundu wa Msimbazi Simba ya kuomba kutumia uwanja wa New Aman sports Comlpex katika michezo ya nyumbani ya Ligi kuu, kombe la shirikisho la Azam (ASFC) na michezo iliyosalia ya hatua ya makundi Klabu Bingwa barani Afrika (CAFCL).

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Visiwani Zanzibar Hussein Ahmada Vuai amesema kuwa leo Januari 29 mwaka 2024 wamepokea barua rasmi kutoka klabu ya Simba ya kuomba kutumia uwanja wa Amani katika michezo yake ya nyumbani kwa mashindano mbalimbali.

“Nikiri kwamba leo ofisi yangu ya katibu Mkuu ZFF nimepokea barua rasmi kutoka kwa Klabu ya Simba ya Dar es Salam kuomba kutumia Uwanja wa New Aman Sports Comlpex katika michezo yake ya nyumbani baada ya Kiwanja cha Mkapa na Uhuru kufungiwa kupisha ukarabati,” amesema.

“Sisi ZFF kwa upande wetu tumepokea barua hiyo kwa heshima kubwa kwa ndugu zetu Timu ya Simba na kwetu sisi tunaona ni jambo linaloweza kuleta faraja kwa mpira wa Zanzibar endapo litakwenda kufanikiwa kwa asilimia 100 na kufungua fursa kwa Wazanzibar na Watanzania wanaoishi visiwani humu kuiona Ligi kuu ya NBC na mashindano mengine kuchezwa Zanzibar,” ameongeza

Amefafanua kwamba, Msimamo wa Shirikisho la Soka Zanzibar kutoa ushirikiano kwa klabu ya Simba ili kufanikisha matakwa yao.

Aidha amefafanua kuwa baada ya kupokea barua amechukua jitihada za kuzungumza na Meneja wa Uwanja, Bodi ya Ligi, Kamshna wa Idara ya Michezo na Wizara yenye dhamana na michezo Visiwani Zanzibar.

“Baada ya kupokea barua sisi kama ZFF Jukumu letu ni kuweza kupeleka taarifa hizi katika vyombo ambavyo tunafanya navyo kazi kwa karibu kwa ajili ya kuweza kufanikisha hili,” ameeleza Hussein Ahmada Vuai.

SOMA NA HII  BALAAH HILI....!! GWIJI GENK AMKATAA SAMATTA HADHARANI...AFUNGUKA A-Z JINSI TIMU ITAKAVYOYUMBA...