Home Uncategorized YANGA YAITUMIA DONGO KIMTINDO SIMBA ISHU YA WACHEZAJI WAKE

YANGA YAITUMIA DONGO KIMTINDO SIMBA ISHU YA WACHEZAJI WAKE


 ANTONIO Nugaz, Ofisa Uhamasishaji wa Klabu ya Yanga amesema kuwa wachezaji wa Simba walicheza chini ya kiwango kwenye mchezo wa dabi jana Novemba 7 kwa kuwa walikutana na wachezaji wenye kiwango bora.


Yanga walikamilisha raundi ya 10 bila kufungwa ndani ya Ligi Kuu Bara waliweza kusepa na pointi moja mbele ya Simba ambayo imepoteza mechi mbili.

Ikiwa chini ya Kocha Mkuu, Cedric Kaze ilianza kufunga bao la kuongoza dakika ya 31 kupitia kwa Michael Sarpong kwa mkwaju wa penalti baada ya Joash Onyango kumchezea faulo Tuisila Kisinda na mwamuzi wa kati Abdalah Mwinyimkuu kuamuru ipigwe penalti.


Simba ilipata bao la kuweka usawa dakika ya 86 kupitia kwa beki Onyango baada ya kumalizia mpira wa kona iliyopigwa na Luis Miquissone wengi hupenda kumuita Konde Boy.


Nugaz amesema:”Kweli Simba imecheza chini ya kiwango kwa kuwa imekutana na timu yenye wachezaji ambao wana kiwango kikubwa zaidi yao.


“Tuliwatamani sana Oktoba 18 tukawakosa ila kwa kuwa walikuja Novemba 7 tulikutana nao ila tumeweza kuona namna gani timu inacheza na mbinu ambazo Kaze yupo nazo.” 

SOMA NA HII  KIKOSI CHA YANGA DHIDI YA TANZANIA PRISONS